Bei ya nafaka imeendelea kupanda licha ya kuongezeka kwa uzalishaji:FAO

Bei ya nafaka imeendelea kupanda licha ya kuongezeka kwa uzalishaji:FAO

Bei ya nafaka duniani imeendelea kupanda licha ya kuwepo kwa chakula cha ziada limesema shirika la chakula na kilimo FAO Alhamisi.

Kwa ujumla bei imepanda kwa zaidi ya asilimia 16 ikilinganishwa na mwezi Januari mwaka jana , na imeongezeka asilimia mbili ikilinganishwa na mwezi uliopita wa Januari.

FAO imesema nafaka zimepanda kwa asilimia 3.4 kutoka Desemba mwaka jana na inaonekana itafikia kiwango cha juu na kuweka rekodi ifikapo mwisho wa msimu wa upanzi mwaka huu.

Bei ya sukari imeongezeka kwa kwa karibu asilimia kumi, kutokana na matarajio kwamba ugavi utabanwa katika nchi zinazozalisha sukari za Brazil, India na Thailand.

Kwa mujibu wa FAO Januari umekuwa ni mwezi wa sita mfulolozo bei ya nafaka inapanda tangu mwaka 2016.