Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia wa Norway ajitolea kuwasaidia wakimbizi

Raia wa Norway ajitolea kuwasaidia wakimbizi

Kulingana na takwimu za Shrika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, zaidi ya watoto milioni 500 duniani wamekimbia makazi yao kutokana na vita na vurugu, wengi wao wakitenganishwa na wazazi wao. Wengi wa manusura wakiweza kutoroka na wazazi wao hukimbilia nchi jirani kusaka hifadhi. Mwaka jana, takriban wakimbizi 140 kutoka Syria na Iraq wamekimbilia mji wa Sandefjod nchini Norway. Katika Makala hii, tunakutana na mmoja wa wakazi wa mji huo, Bwana Frode, aliyejitolea kibinafsi kuwasaidia wakimbizi hao...ungana na Selina Jerobon kuelewa jinsi ukarimu wake unavyomridhisha....