Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tutahakikisha uchaguzi wa wazi na ukweli Somalia

Tutahakikisha uchaguzi wa wazi na ukweli Somalia

Baada ya vuta ni kuvute na dosari katika mchakato wa uchaguzi wa mabunge nchini Somalia, macho yote sasa yanaelekea katika uchaguzi wa Rais utakaofanyika tarehe 8 mwezi huu. Rosemary Musumba na taarifa kamili

(TAARIFA YA ROSE)

Ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini Somalia, AMISOM umesema wagombea 24 watawania kiti hicho cha Rais kwa kupitia kura ya siri itakayopigwa na bunge hilo.

Akihojiwa na AMISOM, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa rais, Abdirahman Beileh amesema Somalia sio nchi pekee ambayo rais anachaguliwa na bunge kwani..

(Sauti ya Abdirahaman)

“Bunge linalochagua rais limechaguliwa na wananchi, kwa hiyo tunawakilisha wananchi, tunawasikiliza, tumeapishwa, na tumetoa ahadi kwamba tutafanya kila tuwezalo, kumchagua mwenye uwezo mkubwa kwa niaba yao, na niwahakikishia watu wa Somalia kwamba tutakuwa waugwana katika dhamira yao, ya nchi na taifa kwa ujumla”.