Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wabunge waungana dhidi ya itikadi kali na ugaidi:UNODC

Wabunge waungana dhidi ya itikadi kali na ugaidi:UNODC

Tishio la ugaidi dhidi ya amani na usalama limeongezeka na kuenea, na linaathiri watu wengi ambao wanarubuniwa kuingia katika ugaidi hasa kupitia mitandao ya kijamii au propaganda za kidini.

Hayo yamejitokeza kwenye mkutano wa kikanda wa wabunge wa nchi za Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini MENA ulioanza Aswan Misri Januari 31 na unakamilika leo Februari pili.

Wabunge wanajadili mitazamo ya kisheria dhidi ya kuzuia ugaidi na itikadi kali inayosababisha ugaidi Katika mkutano huo wa msaada wa kiufundi wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya dawa na uhalifu UNODC, wito umetolewa wa kuwa na uwiano wa mtazamo baina ya hatua za usalama na zile za kuzuia ugaidi.

Miongoni mwa waliozungumza kwenye mkutano huo ni pamoja na Katibu Mkuu wa muungano wa mabunge duniani IPU Bwana Martin Chungong.