Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulaghai katika sekta ya madini ukiepukwa Afrika itanufaika zaidi.

Ulaghai katika sekta ya madini ukiepukwa Afrika itanufaika zaidi.

Shirika la fedha duniani IMF, limesema kuwa bara la Afrika laweza kunufaika zaidi na uwepo wa madini ikiwa mapato ya kodi kwa bidhaa hizo yataongezwa na kuzingatia kanuni ya bei za bidhaa.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na taasisi ya kimataifa ya udhibiti wa rasilimali, na kuhusisha mataifa manne ya Afrika ikwamo Tanzania, Guinea, Ghana na Sierral Leone na Zambia ,ulaghai wa soko la madini ndiyo unaokosesha Afrika fedha toshelevu.

Alexandra Readhead ni mwandishi wa ripoti hiyo na hapa anatolea mfano wa biashara ya madini nchini Guinea.

( Sauti Alexandra)

"Unachimba madini ya chuma kutoka ardhini kwa mfano huko Guinea, na kisha kampuni tanzu ya madini ya Guinea inauza madini hayo kwa kampuni mwenza inayohusika na masoko, na kisha kampuni hiyo inauza bidhaa hizo kwa mawakala, kwa hiyo bei ya uhamisho ni bei ya manunuzi kati ya kampuni ya uchimbaji ya Guinea na kampuni ya masoko ng'ambo, na hapo ndipo panaweza kutumika kama fursa ya kuhamisha faida kutoka Guinea."

IMF inasema nchi zinazoendelea zinapoteza kiasi cha kati ya dola bilioni 100 hadi 300 kwa mwaka, kutokana na ukwepaji kodi katika sekta ya madini.