Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM yaonya ujenzi wa Israel ndani ya maeneo ya wapalestina

UM yaonya ujenzi wa Israel ndani ya maeneo ya wapalestina

Umoja wa Mataifa una wasiwasi mkubwa na tangazo la hivi karibu la serikali ya Israel la kuendeleza ujenzi wa makazi 5,000 katika eneo linalokaliwa la wapalestina la ukingo wa magharibi mwa mto Jordan.

Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu imesema kuwa kitendo hicho kinatishia mpango wa ufumbuzi wa suluhisho la amani kati ya Israel na Palestina.

Kwa mantiki hiyo, ameonya dhidi ya hatua yoyote ambayo itakuwa kizuizi katika mazungumzo ya ufumbuzi wa amani.

Na hivyo amesema Umoja wa Mataifa unatoa wito kwa pande hizo mbili kurejelea mazungumzo ya msingi kwa kulingana na maazimio husika ya Baraza la Usalama na kwa mujibu wa sheria za kimataifa, na kusema kwamba uko tayari kuunga mkono utaratibu huo.