Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Primero kuimarisha ulinzi wa watoto- UNICEF

Primero kuimarisha ulinzi wa watoto- UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na wadau wake wameunda programu ya kompyuta kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano katika juhudi za kuhudumia watoto wakimbizi wa ndani katika nchi zilizokumbwa na mizozo. Taarifa zaidi na John Kibego

(Taarifa ya John Kibego)

Programu hii itwayo Primero, inawezesha ukusanyaji salama wa taarifa, uwekaji na ubadilishanaji wake ili kuimarisha ulinzi wa watoto, ufuatiliaji wa usalama wao, na huduma za kuwaunganisha na familia zao.

Cornelius Williams, ýambaye ni Mkurugenzi wa UNICEF kuhusu ulinzi wa watoto amesema, teknolojia hii mpya itaimarisha uwezo wa serikali na mashirika ya kibinadamu kutambua watoto waliohatarini, kuwapatia huduma za kuokoa maisha na kuwalinda dhidi ya unyonyaji na vurugu.

“Primero” itatumiwa Lebanon, Jordan na kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya, halikadhalika kwingineko ambako huduma hiyo inahitajika"