Skip to main content

Mkuu wa UNMISS apata hakikisho la usalama Wau

Mkuu wa UNMISS apata hakikisho la usalama Wau

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini, David Shearer amefanya ziara kwenye jimbo la Wau nchini humo na kujionea hali halisi ikiwemo wakimbizi 28,000 waliosaka hifadhi kwenye kituo cha Umoja wa Mataifa.

Akiwa ziarani humo, wakuu wa mamlaka za Wau wamemhakikishia kuwa mashirika ya kibinadamu na raia hayatakumbana na vikwazo vyovyote wakati wa shughuli zao.

Naye Bwana Shearer ambaye pia ni mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS akihojiwa na radio Miraya ya umoja huo amesema..

(Sauti ya David)

"Kile kilichonigusa ni kwamba Umoja wa Mataifa na mamlaka wana lengo sawa kwa ajili ya watu takriban 40,000 walioko katika kambi mbali mbali Wau na jinsi ya kurejea makwao, lakini wakati nilizungumza na baadhi ya wakazi wa kambi wanasema kwamba wanachohofia ni usalama wao na nilipozungumza na viongozi na gavana wa eneo hilo niliwaambia kwamba kitu kikubwa kinachohotaji ni usalama na amani."