Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUSCO yafunza wanajamii kulinda rasilimali

MONUSCO yafunza wanajamii kulinda rasilimali

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC , MONUSCO, umefanya mafunzo kwa jamii jimboni Kivu Kusini kuhusu usimamazi wa rasilimali, maendeleo na mabadiliko ya tabianchi.

Kwa mujibu wa wavuti wa MONUSCO, mafunzo hayo kwa wanajamii ambayo yalishirikisha wadau kama vile asasi za kiraia, yamejengea uwezo kamati za maendeleo za serikali za mitaa katika kutunza mazingira kwa kupanda miti na uhakika wa chakula.

Ujumbe huo umeeleza kuwa wakazi wa Uvira wamepiga hatua katika utunzaji wa rasilimali kama vile kulinda ardhi iliyokumbwa na mmomonyoko wa udongo na ukame uliosababisha ukosefu wa chakula utokanao na upungufu wa maeneo ya malisho na mazao.

Mafunzo haya yamekwenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti mwishoni mwa mwezi Januari ambapo lengo ni kupanda miti 10,000 katiak vijiji husika.