Sera kandamizi za afya zarejesha vijana nyuma

1 Februari 2017

Mmoja wa vijana walioshiriki kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu vijana ambalo limekunja jamvi siku ya Jumanne kwenye makao makuu, New York, Marekani amesema sera kuhusu afya ya vijana haziko wazi.

Alvin Mwangi kutoka Kenya anayefanya kazi na shirika la YAS linalofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Ukimwi UNAIDS, ameiambia Idhaa hii wakati wa mahojiano kuwa nchini mwake sera hizo ni baguzi na hivyo kile ambacho angependa kuona ni..

(Sauti ya Alvin)

"Sera zilizo fanisi na jumuishi zenye kuonyesha namna ambavyo kijana anaweza kupata huduma ya afya katika vituo vyovyote, na sisi tungependa iwe yenye kupatikana kiurahisi, yenye bei nafuu na yenye wahudumu waliobobea na vifaa sahihi".

Vijana kutoka nchi mbali mbali walijadili mada wanazozichagiza katika nchi zao sambamba na malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, ikiwa ni pamoja na kubadilishana mawazo na wenzao na kujadiliana na watunga sera.

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.