Skip to main content

Nina matumaini makubwa na sitisho la mapigano Syria: De Mistura

Nina matumaini makubwa na sitisho la mapigano Syria: De Mistura

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa na mashaurio hii leo kuhusu Syria ambapo baada ya kikao mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria Staffan de Mistura amewaambia waandishi wa habari kuwa ana matumaini makubwa kuwa sitisho la mapigano nchini huko litaendelea kudumu zaidi.

Amesema matumaini hayo yanazingatia kwamba hii ni mara ya kwanza vikundi 13 vyenye silaha pamoja na serikali wamekaa pamoja kujadiliana na zaidi ya hapo..

(Sauti ya De Mistura)

Pili ni kwamba kuna nia ya mpango wa utekelezaji ambao haukuwepo hapo awali. Pia kuna nchi tatu Urusi, Uturuki na Iran ambazo ni kama wafadhili na zina uwezo wa kufanya sitisho la mapigano lidumu na tayari zinaonyesha kuwa ziko tayari na kufanyika kwa mkutano mwingine wa kiufundi tarehe Sita Februari ili kubuni njia za kuimarisha sitisho.” 

Kuhusu mkutano wa hivi karibu kuhusu Syria uliofanyika Astana, Kazakstan Bwana de Mistura amesema kuwa japokuwa walikubaliana kufuatilia mazungumzo hayo mwezi tarehe Sita mwezi Februari, yeye amependekeza kuahirishwa hadi tarehe 20 Februari ili kuipatia nafasi kutekelezwa kwa mkataba wa sitisho la mapigano, na pia kuwapa fursa kuleta wawakilishi kutoka pande zote ikiwemo wanawake akitaja kuwa

(Sauti ya De Mistura)

“Itanibidi kutumia mamlaka niliyopewa na azimio 2254 ya kuchagua wawakilishi kwenye kikao kinachokuja. Kuweza kuchagua wawakilish wanawake, ambayo haijawahi kufanyika hapo awali, wapinzani na serikali ili kupeana usawa wa kuzungumzia ajenda ambayo ni azimio namba 2254.”