Skip to main content

Vifo 250 vyaripotiwa Mediteranea mwezi Januari pekee- IOM

Vifo 250 vyaripotiwa Mediteranea mwezi Januari pekee- IOM

Zaidi ya watu 250 wamefariki dunia kwa mwezi huu wa Januari pekee wakivuka bahari ya Mediteranea kuelekea Ulaya.

Msemaji wa IOM Joel Millman amesema miongoni mwao ni watoto wanne wa familia moja kutoka Côte d'Ivoire waliokuwa wanakwenda Ufaransa kuungana na baba yao.

Watoto hao ni wavulana wawili wenye umri wa miaka mitano na minne na wasichana wawili wenye umri wa miaka 10 na 14 .

Walifariki dunia kwa kukosa hewa na maiti walipatikana kwenye boti lisilo thabiti lililolokuwa linatoka Libya kuelekea Italia.