Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi Nyarugusu wapatiwa fedha taslimu-WFP

Wakimbizi Nyarugusu wapatiwa fedha taslimu-WFP

Wakimbizi wapatao 10,000 katika kambi ya Nyarugusu, mkoani Kigoma, nchini Tanzania wanapatiwa fedha taslimu kutoka shirika la mpango wa chakula duniani, WFP ili kujipatia mahitaji ya chakula.

Mradi huo wa majaribio wa miezi mitatu unalenga wakimbizi wenye mahitaji maalum na umewezekana kufuatia mchango wa Canada wa dola 385,000 kwa WFP.

Saidi Johari ni mkuu wa ofisi ya WFP, Kasulu.

(Sauti ya Said)

Amesema mpango huo ambao wanufaika wataongezeka ifikapo mwishoni mwa mwaka huu siyo tu unawezesha wakimbizi kubadili mlo na kupata kile wapendacho bali pia..

(Sauti ya Said)

Hata hivyo katika kipindi chote cha majaribio wakimbizi wataendelea kupata mgao wa mafuta ya kupikia yenye virutubisho na mchanganyiko maalumu wa uji.