Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yahitaji dola bilioni3.3 kuhudumia watoto 2017

UNICEF yahitaji dola bilioni3.3 kuhudumia watoto 2017

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, limezindua ombi la kiasi cha dola bilioni 3.3 kwa mwaka huu wa 2017 ili kutoa huduma za msingi kwa watoto katika nchi 48 duniani. Amina Hassan na taarifa kamili.

(TAARIFA YA AMINA)

Kwa mujibu wa UNICEF, ombi la kiasi hicho cha fedha ni kwa ajili ya huduma kama vile maji safi, virutubisho,elimu na afya, ambapo watoto milioni 48 wanaoshi katika maeneo yenye mizozo watanufaika.

Nchi ambazo watoto wanakabiliwa na mashambulizi ya moja kwa moja ni pamoja na Yemen, Iraq, Sudan Kusini, na Nigeria.

Manuel Fontaine ni Mkurugenzi wa masuala ya dharura wa UNICEF anasema majanga ya asili na mabadiliko ya tabianchi yanawashinikiza watoto kuhama majumbani, huwapeleka vitani, na hukabiliwa na magonjwa kama unyafuzi.

(Sauti Manuel)

‘Tunakadiria kwamba watoto milioni saba na nusu watakabiliwa na unyafuzi ifikapo baadae mwaka huu, kama unavyofahamu unyafuzi waweza kusababisha kifo.’’

 Raymond Johnson ni mtoto wa miaka 18 aliyeko kambini nchini Sudan Kusini anaeleza madhila anayokumbana nayo ikiwamo majinamizi usiku.

(Sauti Raymond)