Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatiwa hofu na athari za kusitishwa mpango wa wakimbizi Amerika:

UNHCR yatiwa hofu na athari za kusitishwa mpango wa wakimbizi Amerika:

Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Filippo Grandi, amesema anatiwa hofu kubwa na hali ya sintofahamu inayowakabili maelfu ya wakimbizi kote duniani ambao wako katika mchakato wa kupewa makazi Marekani.

Wiki hii pekee zaidi ya wakimbizi 800 walitakiwa kuifanya Marekani kuwa makazi yao mapya, badala yake wamejikuta wakipigwa marufuku ya kuingia Marekani .

UNHCR inakadiria kuwa wakimbizi 20,000 walio katika mazingira magumu wangeweza kupewa maskani nchini Marekani wakati wa siku 120 za usitishaji wa mpango wa wakimbizi, usitishaji uliotangazwa na serikali ya Marekani kuanzia Ijumaa iliyopita. UNHCR inasema idadi ni wastani wa kila mwezi kwa miaka 15 iliyopita.

Imeongeza kuwa kwa wakimbizi wamejikuta kuwa na shauku, kuchanganyikiwa na kuvunjika moyo na usitishaji huo ambao tayari ni mchakato mrefu.

Wakimbizi kwa mujibu wa UNHCR pia wanahofia ulinzi na usalama kama serikali ya Marekani kwani wao pia wanakimbia vita, mauaji, ukandamizaji na ugaidi.