Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuimarisha utawala ni muhimu katika ukuaji wa maendeleo nchi zinazoendelea

Kuimarisha utawala ni muhimu katika ukuaji wa maendeleo nchi zinazoendelea

Ripoti mpya ya sera ya Benki ya dunia imezitaka nchi zinazoendelea na mashirika ya kimataifa ya maendeleo kufikiria upya mtazamo wao dhidi ya utawala kama kiungo muhimu cha kukabiliana na changamoto zinazohusu usalama, ukuaji na usawa.

Ripoti hiyo ya maendeleo duniani mwaka 2017 inajikita katika “utawala na sheria kutathimini jinsi gani usambazaji usio sawia wa madaraka katika jamii unavyoingilia utekelezaji wa sera.

Benki ya dunia inasema kutokuwepo mlingano wa madaraka kwa mfano kunaweza kuelezea ni kwa nini mara nyingi sheria na mashirika ya kukabiliana na ufisadi yanashindwa , na kwa nini kutoa madaraka kwa wananchi hakusaidii kuboresha manispaa au ni kwa nini sera nzuri zinaweza zisipunguze msukosuko na kusaidia akiba ya muda mrefu.

Ripoti hiyo pia imeanisha kwamba wakati sera na suluhu za kiufundi zinaposhindwa kutimiza malengo taasisi ndizo zinazolaumiwa mara nyingi. Hata hivyo ripoti hiyo imebaini kwamba nchi na wahisani wanapaswa kufikiria kwa mapana zaidi kuimarisha utawala ili sera ziweze kufanikiwa