Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutoka kuishi kwenye mahame hadi hotelini

Kutoka kuishi kwenye mahame hadi hotelini

Huko Ugiriki, usaidizi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR umewezesha wakimbizi waliokuwa wamesaka hifadhi kwenye mabohari yaliyotelekezwa kuhamishiwa maeneo bora yenye huduma za msingi. Hii inakuja baada ya maombi kutoka jumuiya ya kimataifa ya kutaka wahamishwe kwa kuwa walikuwa wanaishi kwenye mazingira magumu, kwa kuzingatia baridi kali na hawana vifaa vya kuwawezesha kutia joto makazi yao. Je nini kilifanyika? Ungana basi na Assumpta Massoi kwenye makala hii.