Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola milioni 100 kusaidia nchi zenye majanga: Guterres

Dola milioni 100 kusaidia nchi zenye majanga: Guterres

Umoja wa Mataifa leo umetoa kiasi cha dola milioni 100 kupitia mfuko wa mwitikio wa dharura CERF, ili kuendeleza operesheni za usaidizi katika nchi ambazo majanga yake hayajapewa kipaumbele.

Taarifa ya Umoja huo kuhusu fedha hizo, imemnukuu Katibu Mku wake António Guterres akisema kuwa uwezeshaji huo ni muhimu ili UM na wadau waendelee kusaidia watu wenye uhitaji mkubwa zaidi, huku pia akiwashukuru nchi wahisani waliowezesha.

Zaidi ya watu milioni sita wanatarajiwa kunufaika kupitia fungu hilo la CERF, ambapo kati ya tisa, nane zatoka barani Afrika ambazo ni Uganda, Somalia Madagascar, Nigeria, Nigeria Mali, Libya na Cameroon. Nchi pekee iliyoko nje ya bara hilo ni Jamhuri ya watu wa Korea.

Zaidi ya watu milioni 65 duniani kote, wamefurushwa kutokana na mizozo.