Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamilioni wanakabiliwa na uhaba wa chakula Pembe ya Afrika-FAO

Mamilioni wanakabiliwa na uhaba wa chakula Pembe ya Afrika-FAO

Wakati robo tu ya mvua ndio iliyonyesha katika msimu wa masika wa Oktoba hadi Desemba mwaka jana kwenye Pembe ya Afrika hivi sasa ukame umeshamiri eneo hilo limesema shirika la chakula na kilimo FAO. Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Shirika hilo linakadiria kwamba zaidi ya watu milioni 17 hivi sasa wako katika mgogoro na hali ya dharura ya uhaba wa chakula katika nchi zilizo chini ya mwamvuli wa IGAD ikiwemo Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Somalia, Sudan Kusini, Sudan na Uganda, ambazo sasa zinahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu.

Kwa mujibu wa FAO maeneo yanayotia hofu zaidi ni Somalia, Kaskazini Mashariki na Pwani ya Kenya, Kusini Mashariki mwa Ethiopia pamoja na jimbo la Afar ambalo bado athari za El Nino za 2015/16 hazijaisha; kwingine ni Sudan Kusini na jimbo la Darfur Sudan kutokana na matatizo ya muda mrefu ya kutokuwepo usalama.

Hivi sasa karibu watu milioni 12 Somalia, Ethiopia na Kenya wanahitaji msaada wa chakula .