Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika yahifadhi wakimbizi licha ya changamoto lukuki: Guterres

Afrika yahifadhi wakimbizi licha ya changamoto lukuki: Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelisifu bara la Afrika kwa kuendelea kuhifadhi wakimbizi licha ya bara hilo kukabiliwa na madhila kadhaa. Flora Nducha na maelezo kamili.

( TAARIFA YA FLORA)

Akizungumza wakati wa mkutano wa Muungano wa Afrika unaondelea mjini Addis Ababa nchini Ethiopia, Guterres amesema bara hilo sio tu kwamba linahifadhi wakimbizi lakini pia linatoa walinda amani wengi kuliko bara jingine duniani.

Kuhusu uhifadhi wa wakimbizi na wasaka hifadhi amesema.

( Sauti Guterres)

‘‘Mataifa ya Afrika pia ni miongoni mwa nchi kubwa kwa ukarimu na uhifadhi wa wakimbizi. Mipaka ya Afrika inasalia wazi kwa wale wanaohitaji ulinzi, wakati ambapo mipaka mingi imefungwa, hata katika nchi zilizoendelea zaidi duniani.’’

Kuhusu ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Afrika, Katibu Mkuu amesema anakaribisha mawazo ya namna ya kuimarisha ushirikiano na ubia katika vipaumble na mahitaji ya watu wa Afrika hususani ni.

( Sauti Guterres)

‘‘Kwanza, kuinua kiwango cha ubia wa kimkakati katika kutekeleza ajenda 2063 na ile ya 2030, na katika kukuza amani na usalama na haki za binadamu pamoja.’’