Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kituo cha utekelezaji wa SDG’s Afrika chazinduliwa Rwanda

Kituo cha utekelezaji wa SDG’s Afrika chazinduliwa Rwanda

Katika juhudi za kuhakikisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu (SDG’s) barani Afrika kituo maalumu cha kuhakikisha hilo limezinduliwa Ijumaa mjini Kigali Rwanda.

Zaidi ya viongozi wa kimataifa 200 kutoka serikalini, makampuni ya biashara, wa nazuoni na asasi za kiraia wamekusanyika mjini Kigali kushughudia uzinduzi huo wa kihistoria wa SDG centrer for Africa (SDGC/A) ambacho kitakuwa makao makuu.

Malengo ya maendeleo endelevu yalipitishwa na baraza kuu la Umoja wa Mataifa Septemmba 2015. Akizungumzia kuhusu Rwanda katika uzinduzi huo Rais Paul Kagame amesema

(SAUTI YA KAGAME 1)

“Kwa Rwanda mtazamo wa kujadiliana na kushirikisha kila upande umekuwa ndio chachu ya mafanikio na hatua tuliyopiga ,lakini siku zote tunaweza kuongeza juhudi na kufanya vizuri zaidi.”

Ameongeza kuwa malengo hayo ni kipimo kwa uongozi wa nchi

(SAUTI YA KAGAME 2)

“Malengo ya SDG’s yanatoa fursa pekee ya kudhihirisha siasa nzuri, na kuyafanya yaeleweke zaidi kama kigezo cha kujumuisha wote katika maendeleo endelevu. Malengo haya yasionekane kama ni ajenda kutoka nje , bali kama sehemu ya nchi ya mtazamo wa maendeleo”