Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlipuko wa PPR miongoni mwa Swala watia hofu: FAO

Mlipuko wa PPR miongoni mwa Swala watia hofu: FAO

Ugonjwa unaoua kwa kasi mifugo ujulikanao kama Peste des Petitis au PPR ndio uliobainika kuwa sababu ya vifo vya swala adimu nchini Mongolia. Takribani swala 900 wamekutwa wamekufa Mashariki mwa Mongolia kwenye jimbo la Khovd. Idadi hiyo ni takribani asilimia 10 swala hao.

Ugonjwa wa PPR unajulikana kwa kuathiri zaidi mbuzi na kondoo kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo FAO mlipuko wa sasa miongoni mwa swaqla unatia hofu kwa wataalamu kama anavyoeleza zaidi Dr Juan Lubroth mkuu wa kitengo cha mifugo wa FAO.

(SAUTI YA DR LUBROTH)

"Sasa fikiria kwamba nchini Mongolia maeneo ya kulisha mifugo ni machache kwa hiyo utakuta kwamba swala, mifugo na wachungaji wanakutana hivyo hapo kunaweza kutokea maambukizi."