Nchi zisiogope kutekeleza haki za watu wa asili

26 Januari 2017

Nchi zisiogope kuimarisha haki za watu wa asili kama zilivyoainishwa na azimio la Umoja wa Mataifa lililopitishwa muongo mmoja uliopita a. Wito huo umetolewa na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa asili.

Victoria Tauli Corpuz amesema azimio lililopitishwa 2007 ni mkusanyiko wa machozi na malalamiko yaliyowasilishwa na watu wa asili kwa viongozi wa dunia.

Kuna zaidi ya watu wa asili milioni 370 kote duniani kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ambao ni asilimia 15 ya watu wote wanaoishi katika umasikini.

Bi Corpuz ana ujumbe huu

(SAUTI YA CURPUZ)

“Kwa watu wa asili kutumia vyema mafanikio waliyoyapata katika kuhakikisha haki za watu wa asili zinatambuliwa kitaifa, kimataifa na kwenye mfumo wa Umoja wa Mataifa, kujiimarisha na kujiwezesha na kulifanya mashirika kudai utekelezaji wa azimio hilo.”

Na kwa upande wa serikali

(SAUTI YA CURPUZ)

“Ujumbe wangu ni kwa wao kutambua kwamba endapo wataheshimu haki za watu wa asili watakuwa na fursa bora ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo kitaifa, watakuwa na fursa nzuri ya kuokoa mazingira katika nchi zao, na wasiogope kutekeleza haki za watu wa asili kwani mwisho wa siku ni muhimu kwa jamii na kwa dunia nzima kwa ujumla”

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter