Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR -Tumesikia tangazo la Amerika kujenga ukuta mpakani na Mexico:

UNHCR -Tumesikia tangazo la Amerika kujenga ukuta mpakani na Mexico:

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linazingatia tangazo la serikali ya Marekani la nia ya kutaka kujenga ukuta kwenye mpaka wake na Mexico.

Shirika hilo limesema litafuatilia kwa karibu athari za uamuzi huo kwa watu wanaoomba hifadhi ya ukimbizi nchini Marekani. Pia itaendelea kushirikiana kwa karibu na serikali ya Marekani kama inavyofanya kwa miongo kadhaa sasa.

UNHCR imeongeza kuwa katika wakati huu wa mahitaji makubwa ya kuwalinda wakimbizi inatuamai kwamba Marekani itaendelea na uongozi wake imara na utamaduni wa muda mrefu wa kuwalinda wale wanaokimbia vita na mauaji.