Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF, EU kusaidia zaidi ya watoto wakimbizi 6,000 Ugiriki

UNICEF, EU kusaidia zaidi ya watoto wakimbizi 6,000 Ugiriki

Ushirikiano kati ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na jumuiya ya Ulaya EU, utasaidia zaidi ya watoto wakimbizi na wahamiaji 6,000 nchini Ugiriki, wanaopitia kwenye hali ngumu.

Kwa mujibu wa UNICEF, mradi huo wenye thamani ya Euro milioni nane na nusu, zinazofadhiliwa na kitengo cha cha misaada ya dharura cha EU, utawanusuru watoto katika elimu, ulinzi hususani wakati huu ambapo kuna hali mbaya ya hewa.

Mradi huu utashughulikia kuziba mapengo muhimu katika kuhakikisha watoto wanaohama na familia zao wanalindwa, wanakuwa salama na wanaweza kuhisi wako kawaida, imesema UNICEF.

Rula Manan ni mtoto msaka hifadhi nchini Ugiriki.

(Sauti Rula Manan)

‘‘Tangu tumekuja hapa, muda mwingi tumekabiliwa na hofu. Tunaogopa na tumechoka. Hii ni zaidi ya kuchoka’’

UNICEF inakadiria kuwa kuna watoto wakimbizi zaidi ya 21,000 nchini Ugiriki, wengi wao wakikabiliwa na athari za kisaikolojia kutokana na adha wanazozipitia.