Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wawe makini na propaganda chafu- Wanafunzi

Vijana wawe makini na propaganda chafu- Wanafunzi

Nchini Tanzania leo kumefanyika kumbukizi ya siku ya kimataifa ya mauaji ya halaiki au Holocaust ambapo vijana wamepata fursa ya kuelimishwa jinsi propaganda ikitumiwa vibaya inaweza kuleta mgawanyiko na madhara ulimwenguni.

Shughuli hiyo iliandaliwa kwa pamoja na pande kadhaa ikiwemo kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, UNIC, Ubalozi wa Ujerumani, Shule za Sekondari na vijana ambao hawapo shuleni ambapo Afisa wa ubalozi wa Ujerumani Susan Keller amesema anajutia uhalifu uliotendwa na wajerumani dhidi ya wayahudi na makundi mengine.

Akigusia athari za propaganda, Kalista Richard ambaye ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Jitegemee amesema..

(Sauti ya Kalista)

Naye Salim Omari Manga kutoka shule ya sekondari Airwing amesema..

(Sauti ya Salim)

Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumbukizi ya mauaji ya halaika itafanyika kesho Ijumaa ambapo maudhui yanalenga kuelimisha umma jinsi propaganda chafu zinavyoweza kuleta madhara kwenye jamii.