Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tutaendelea kuwa bega kwa bega na CAR- Lagarde

Tutaendelea kuwa bega kwa bega na CAR- Lagarde

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la fedha duniani, IFM Christine Lagarde, leo anahitimisha ziara yake ya siku mbili nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR ambako amekuwepo kwa ajili ya kutathmini mapendekezo ya shirika hilo yenye lengo la kukwamua uchumi wa nchi hiyo.

Bi. Lagarde ambaye amekuwa na mazungumzo na Rais Faustin-Archange Touadera  wa CAR na wabunge wa amewaeleza waandishi wa  habari mjini Bangui kuwa..

(Sauti ya Lagarde)

“Shirika la fedha duniani limeazimia kutoa rasilimali, na ushauri kwenye nchi zilizo katika hali tete ili kuendeleza uwezo wao wa kupatia suluhu matatizo yanayowakabili. Tunaweza kusaidia CAR. Tumefanya hivyo katika mazingira mengine kama kule Rwanda, Liberia na Msumbiji, nchi ambazo nazo zimepitia changamoto au mzozo baada ya vita na zimerejea kwenye mwelekeo wa maendeleo na maridhiano. Ni safari ndefu lakini ni njia ambayo tunaweza kuwa nao bega kwa bega na tuko tayari kuwa pamoja na CAR.”

Hii ni sehemu ya kwanza ya ziara yake barani Afrika itakayompeleka pia Uganda na Mauritius.