UNIDO na washirika kuwapa ajira zaidi ya vijana 6,000 Tunisia

UNIDO na washirika kuwapa ajira zaidi ya vijana 6,000 Tunisia

Shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda UNIDO, shirika la Marekani la maendeleo ya mkimataifa (USAID), Ushirikiano wa maendeleo wa Italia na mfuko wa HP Jumatano wamezindua awamu ya pili ya mradi wa UNIDO wa ajira kwa vijana ujulikanao kama “My project 3) ukiwa na lengo la kuzalisha nafasi za ajira zaidi ya 6000 kwa vijana nchini Tuniasia katika miaka mitano ijayo.

Hivi sasa katika majimbo ya Katikati, Kusini na Kaskazini mwa Tuniasia asilimia 40 ya vijana waliohitimu shahada na stashahada za juu wameshindwa kupata ajira.

Hali hii inachangiwa na sababu nyingi ikiwemo uwezo mdogo wa sekta za umma kuajiri vijana wanawake na wanaume, kutokuwepo fursa nyingi katika sekta binafsi nan a kutooaana baiana ya ujuzi unaotakiwa na sekta binafsi na ule walionao wahitimu.

Mradi huu ni ishara ya muendelezo wa ushirika wa mafanikio ya kuwapa vijana wa Tuniasia fursa ya kupata kazi.