Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watoa wito wa kuachiliwa watetezi watano wa haki za binadamu Cambodia

UM watoa wito wa kuachiliwa watetezi watano wa haki za binadamu Cambodia

Wataalam wawili wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo wametoa wito kwa serikali ya Kifalme ya Cambodia kuwaachilia haraka watetezi watano wa haki za binadamu ambao wamekuwa kizuizini tangu Mei mwaka jana kwa tuhuma zinazohusiana na msaada waliompatia mwanamke mmoja anayedaiwa kuwa alishinikizwa na idara ya rushwa kutoa madai ya uongo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Geneva, Uswisi mashtaka yalionekana kama masuala ya kisiasa na mwezi Novemba 2016, kikundi wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu vizuizi vya kiholela walilitoa uamuzi kuwa watu hao waloikuwa wanashikiliwa 'holela'.

Mtaalamu maalum Rhona Smith amesema matumizi ya makosa ya jinai kama kisingizio cha kukandamiza na kuzuia zoezi halali la haki ya uhuru wa kujieleza na kunyamazisha watetezi wa haki za binadamu ni kinyume na kifungu cha 19 cha mkataba wa kimataifa wa haki za kiraia na za kisiasa.

Wataalamu hao  wameomba maelezo ya kina kuhusu msingi wa kisheria kwa kizuizi cha  wafanyakazi hao wanne wa haki za binadamu wa shirika la Cambodia lisilo la serikali wakiwa ni -Lim Mony, Ny Vanda, Ny Sokha na Yi Soksan na vile vile naibu katibu mkuu wa kamati ya taifa ya uchaguzi Ny Chakrya.

Wataalam hao wanajiunga na jumuiya ya kimataifa na mashirika ya kiraia katika kutoa wito wa kuachiliwa mara moja kwa wanaharakati hao. Pia wameitaka serikali kuhakikisha kazi ya mahakama nchini humo iko huru.