Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNMISS akutana na Rais wa Sudan Kusini

Mkuu wa UNMISS akutana na Rais wa Sudan Kusini

Mwakilishi mpya wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini , David Shearer amekutana na Rais Salva Kiir wa nchi hiyo. Wakati wa mkutano wao kwenye ofisi ya Rais mjini Juba Bwana.

Shearer, ambaye pia ni mkuu wa mpango wa Umoja wa mataifa nchini humo UNMISS amerejelea kauli yake ya kuwaunga mkono watu wa Sudan Kusini katika juhudi za kuleta amani ya kudumu.Kisha akazungumza na waandishi wa habari

(SAUTI YA SHEARER)

“Kama mtu mpya niliyekuja , nimekuja na mtazamo wa wazi na hivyo nilikuwa radhi kuzungumza na Rais na kusikia kile alichotaka kusema. Nilisisitiza kwake kwamba Umoja wa Mataifa na UNMISS uko hapa kukusaidia watu na kazi yangu itakamilika wakati UNMISS wanaweza kuondoka na kwamba itakuwa jambo bora, tutayaacha nyuma mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo yana uwezo wa kutoa msaada wa kiufundi. UNMISS kama nilivyosema awali tutafanya kila tuwezalo kuisaidia serikali na na watu "

Na baada ya mkutano huo na waandichi wa habari balozi John Andruga, kutoka ofisi ya Rais akatangaza kwamba Salva Kiir atakutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa António Guterres kandoni mwa mkutano wa Muungano wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Mkutano huo ambao tayari umeshaanza katika ngazi ya mawaziri , utawakutanisha wakuu wa nchi tarehe 30 na 31 mwezi huu na Balozi Andruga amesema serikali ya Sudan Kusini imepokea mwaliko maalumu

(SAUTI YA BALOZI ANDRUGA)

“Rais amekubali mwaliko kutoka kwa Katibu Mkuu wa kukutana naye kandoni mwa mkutano wa Muungano wa Afrika Addis,na Rais amethibitisha kwamba atakutana na Katibu Mkuu mpya mjini Addis. Kwa hakika tunahitaji kubadili simulizi na tunahitaji mwanzo mpya, ili watu wa Sudan Kusini wafungue ukurasa mpya na Umoja wa Mataifa. Hatuhitaji kujikita kwenye yale mabaya , tunahitaji kujikita kwenye mambo mazuri , j ya jinsi gani serikali na Umoja wa mataifa wanaweza kufanya kazi pamoja kuwanusuru watu wa Sudan Kusini"