Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Benki ya Dunia yasifu Tanzania na mradi wa BRT

Benki ya Dunia yasifu Tanzania na mradi wa BRT

Nchini Tanzania leo kumefanyika uzinduzi wa awamu ya kwanza ya mradi wa usafiri wa haraka wa mabasi, BRT uliotekelezwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia kwa lengo la kuondoa msongamano wa magari na hivyo kuharakisha huduma na ustawi wa jamii.

Akizindua mradi huo jijini Dar es salaam, Rais wa Tanzania John Magufuli ameshukuru benki hiyo na kuomba ifanikishe mchakato wa mkopo wa ujenzi wa barabara za juu na kwa wasimamizi wa BRT..

(Sauti ya Magufuli)

Naye Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Makhatar Diop amesema BRT imeanza kuleta nuru maeneo ambako inapita na kwa kuwa ifikapo mwaka 2050 nusu ya idadi ya watu wa Tanzania watakuwa wanaishi mijini ..

(Sauti ya Diop)

“Kwa hiyo kuchukua hatua ili kuweka usafiri ambao unakidhi uhalisia huu ni jambo la kuona mbali na hivyo tunapongeza serikali kwa kutambua mahitaji hayo mapema na kubadili mwenendo wa maisha ya watu.”