Uwekezaji binafsi zaidi utasaidia watu wa vijijini: IFAD

Uwekezaji binafsi zaidi utasaidia watu wa vijijini: IFAD

Uwekezaji zaidi kutoka sekta binafsi sanjari na ule wa sekta ya umma utatoa mustakhbali bora kwa watu wa vijijini.

Hiyo ni moja na ajenda muhimu zitakazotamalaki kwenye mkutano wa siku mbili unaoanza leo Jumatano mjini Roma ukijikita katika masuala ya maendeleo ya uchumi vijijini, mwenyeji wa mkutano huo ukiwa ni mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD.

Mkutano huo wa kimataifa “Uwekezaji wa mabadiliko jumuishi vijijini:mtazamo bunifu na ufadhili” unafanyika katika juhudi za kufikia ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu, katika kuwasaidia wakulima wadogowadogo kote duniani.

Mkurugenzi wa ushirikiano wa kimataifa wa IFAD ni Ashwani Muthoo

(SAUTI YA ASHWANI)

“Tunataka kutumia mkutano huu kama jukwaa la kutanabaisha umuhimu wa uwekezaji sio tuu kutoka sekta za umma, lakini hususani kutafuta njia za kujumuisha sekta binafsi, mifuko ya kimataifa na wadau wengine na mashirika ili wawe sehemu ya mchakato wa mabadiliko na kuwekeza katika kubadili maisha ya vijijini”