Kila mwanadamu awajibike kulinda mazingira:UNEP

25 Januari 2017

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP Erik Solheim amesema kuwa kila mwanadamu anawajibu na jukumu la kulinda mazingira na dunia. Akihojiwa na idhaa hii ameongeza kwamba ni muhimu kujihusisha na maslahi ya raia na wakati huo huo katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ni lazima kufanya kazi na sekta binafsi na wafanyibiashara.

(Sauti ya Solheim)

"Tunahitaji kuoanisha maendeleo na mazingira, wakati umepita wa masuala haya mawili kuwa tofauti. Ni lazima kubadilisha tabia na kukuza uchumi unaojali mazingira ili kuongeza ajira. Hapa Tanzania nilipo kwa sasa nimeona kuna changamoto nyingi zinazohusiana na taka na hii inaweza kubadilishwa na kuleta faida ya biashara ya makampuni kufaidika"

Ametoa wito kwa kila mtu kushug hulia mazingira akiongeza kuwa...

(Sauti ya Solheim)

"Raia wana jukumu la kuwasaka wanasiasa wao na kuwawajibisha ili kuleta uchumi unaojali mazingira. Na pili kufanya hivyo kwenye jamii wanazoishi kama vile hapa Tanzania raia sasa wanaenda ufukweni na kuokota taka, na kusafisha ili watu wanaweza kutembelea jambo ambalo ilikuwa halifanyiki hapo awali. Hii ni dunia moja na sote lazima tuishughulikie kwa pamoja"

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter