Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wazima lazima kuwafunza vijana kuheshimu sheria katika vita dhidi ya rushwa: IMF

Watu wazima lazima kuwafunza vijana kuheshimu sheria katika vita dhidi ya rushwa: IMF

Vijana wanaathirika na ufisadi katika njia ya kipekee, na watu wazima wana wajibu wa kuwafundisha jinsi gani ya kuheshimu sheria.

Huo ni mtazamo wa Sergejus Muravjovas anayeongoza shirika lijulikanalo kama Transparency International nchini Lithuania, na pia ni mtoa mada wa mikutano ya kila mwaka ya shirika la fedha duniani IMF na Bank ya dunia.

Alianzisha shule ya kupambana na ufisadi kwa viongozi vijana nchini Lithuania na anasema , hukumu za mapema zinaweza kusambaratisha kabisa maisha ya vijana ya kitaaluma katika jamii nyingi. Hapa anafafanua ni vipi ufisadi unaathiri vijana.

(SAUTI YA SERGEJUS)

“Unakwambia ni fursa zipi ulizonazo, kama unataka kufanikiwa , kama unataka kucheza na sheria, mara nyingi ufisadi haukuruhusu kufanya hivyo, na unakufanya kukubaliana na vitu vingi ambavyo havikuridhishi. Hivyo nadhani kwa mtu yeyote anayetoka katika kiapato cha wastani, au mtu yeyote ambaye anaamini kwamba akijitahidi atafanikiwa , ufisadi ni suala la kutia hofu kwa sababu unawaruhusu wale wenye upenyo na kufahamiana na watu kufanikiwa na wale wanaotoa jasho lao kuambua patupu.”