Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kyrgyzstan-Kuthibitisha kifingo cha maisha kwa mwanaharakati inasikitisha

Kyrgyzstan-Kuthibitisha kifingo cha maisha kwa mwanaharakati inasikitisha

Uamuzi wa kushikilia hukumu ya kifungo cha maisha dhidi ya mwanaharakati wa masuala ya siasa na mwandishi wa habari nchini Kyrgyzstan umeelezewa na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kwama ni wa kusikitisha.

Azimjan Askarov amepatikana na hatia ya makossa kadhaa ikiwa ni pamoja na kushiriki mauaji, uchochezi wa chuki baina ya makabila na utekaji nyara katika mazingira ya ghasia za kikabila kusini mwa nchi hiyo mwaka 2010.

Mahakama ya kitaifa ilikuwa inasikiliza upya kesi yake kwa miezi mitatu iliyopita lakini leo Jumanne imethibitisha uamuzi wa awali wa hukumu ya kifungo cha maisha jela. Ofisi ya haki za binadamu imetoa taarifa isemayo hukumu hiyo haikuzingatia mtazamo wa wataalamu huru wa haki za binadamu ambao walibaini kwamba bwana Askarov alikuwa anashikiliwa kinyume cha sheria, aliteswa na alizuiwa kuandaa utetezi wake.

Pia Mahakama hiyo haikufuatilia madai ya kuteswa Askarovu n ahata mashahidi iliowatumia ni walewale wa kwenye kesi ya awali.