Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama latoa wito kwa serikali ya Sudan Kusini

Baraza la Usalama latoa wito kwa serikali ya Sudan Kusini

Baraza la Usalama limetoa wito kwa serikali ya Sudan Kusini kuongeza juhudi katika ushirikiano baina yake na Umoja wa Mataifa, hususan kuruhusu kupeleka kikosi cha ulinzi cha kikanda nchini humo haraka na kukomesha vizuizi dhidi ya Ujumbe wake, UNMISS.

Wito huo ulitolewa jana jioni baada ya baraza hilo kujadili hali nchini Sudan Kusini, na kutoa msisitizo kwa mamlaka ya nchi hiyo kuhusu umuhimu wa kukomesha ukatili ili kuendeleza amani na kuupa Umoja wa Afrika motisha ya kuanzisha mahakama ya mseto nchini humo.

Rais wa Baraza la Usalama Oloof Skoog aliyeongoza kikao hicho akawaambia waandisha habari jijini New York kuwa..

(Sauti ya Skoog)

"Wajumbe wa Baraza wanawasiwasi mkubwa na kuendelea kwa mapigano nchini Sudan Kusini na kuzuiliwa kwa watoa misaada ya kibinadamu kufanya kazi yao katika maeneo mengi ya nchi ambapo watu wa Sudan Kusini wanateseka na wito kwa wadau wote wa uhasama kusitisha mapigano na kuruhusu upatikanaji wa msaada wa kibinadamu."