Skip to main content

Maendeleo yasiyo jumuishi ni chachu ya migogoro:Guterres

Maendeleo yasiyo jumuishi ni chachu ya migogoro:Guterres

Baraza kuu la Umoja wa mataifa Jumanne li mekuwa na kikao maalumu kujadili ujenzi wa amani kwa wote kwa kuzingatia ajenda yam waka 2030 ya maendeleo endelevu, kama daraja la amani ya kudumu.

Akizungumza katika mjadala huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema maendeleo yoyote yasio jumuishi ni chachu ya migogoro katika jamii

(GUTERRES CUT 1)

“Kuna uhusiano bayana baina ya kushindwa kiuchumi na uwezekano wa mivutano ya kijamii, taasisi n ahata nchi, na matokeo yake tunaona kuzuka kwa mizozo na ile ya awali kutoshughulikiwa”

Na mantiki hiyo ili kuhakikisha amani ya kudumu duniani amesema

“Tunahitaji mwitikio wa kimataifa ambao utashughulikia miziz ya migogoro, na kujumuisha amani, maendeleo endelevu na haki za biandamu katikia njia muafaka, kutoka katika dhana na kuwa vitendo”