Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkurugenzi wa WFP, atembelea waathirika wa Boko Haram

Mkurugenzi wa WFP, atembelea waathirika wa Boko Haram

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, Ertharin Cousin, amewasili nchini Nigeria kwa ajili ya ziara yake Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo amabako WFP, inasaidia waathirika zaidi ya milioni moja wa mashambulio ya wanamgambo wa Boko Haram. John Kibego na taarifa kamili.

(Taarifa ya Kibego)

Baada ya kukutana na maafisa wa serikali na wale wa Umoja wa Mataifa katika Mji Mkuu, Abuja, Bi. Cousin ameelekea kwenye mji wa Maiduguri, kukutana na wanufaika wa operesheni za WFP, wafanyakazi wa shirika hilo, na wadau wote waanaosaidia katika mzozo uliosababishwna kundi la Boko Haram’

Mzozo baina ya serikali na wapiganaji wa Boko Harama umeacha watu takribani milioni mbili wakihitaji msaasa wa dharura, wakati huu ambapo WFP, inapanga kufikisha msaada kwa watu zaidi ya milioni moja waliofikiwa mnamo Disemba mwaka jana Kaskazini mwa Nigeria.

Atahitimisha ziara yake kwa mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa mjini Abuja.