Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya dola bilioni 4 zahitajika kuendelea kusaidia wakimbizi wa Syria:UM

Zaidi ya dola bilioni 4 zahitajika kuendelea kusaidia wakimbizi wa Syria:UM

Mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali leo Jumanne wametoa ombi jipya la dola bilioni 4.63 ili kuweza kuendelea na kazi muhimu ya kushughulikia mahitaji ya wakimbizi kutoka Syria na jamii zinazowahifadhi katika nchi jirani.

Umoja wa Mataifa na mashirika wadau 240 wamezindua ombili rasmi mjini Helsink Finland , katika mkutano maalumu wa kuisaidia Syria, kama mpango maalumu wa wakimbizi ujulikanao 3RP wa mwaka 2017 na 2018.

Mpango huo unalenga kuwasaidia zaidi ya wakimbizi milioni 4.7 kutoka Syria na milioni 4.4 watu kutoka jamii zinazowahifadhi nchini Uturuki, Lebanon, Jordan, Iraq na Misri. Stephen O’Brien ni mratibu wa masuala ya dharura wa Umoja wa Mataifa

(SAUTI YA STEPHEN O'BRIEN )

"Kitu cha msingi cha kutambua Syria ni kwamba licha ya kuwa takribani miaka sita ya visa urefu sawa na vita ya pili ya dunia , mzozo wa Syria unasalia kuwa moja ya mizozo migumu, tete na katili duniani,bila shaka tunahofia kwamba , utakuwa mbaya zaidi, na hata kama amani itapatikana usiku huu, mahitaji ya kibinadamu ndani ya Syria yataendelea kwa muda mrefu ujao"