Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF na UNHCR kuwawezesha vijana wakimbizi kwa teknolojia ya SMS

UNICEF na UNHCR kuwawezesha vijana wakimbizi kwa teknolojia ya SMS

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF na  la kuhudumia wakimbizi UNHCR wameweka saini mkataba wa makubaliano ya kutumia teknolojia ya simu za rununu kuwezesha vijana wakimbizi nchini Pakistan .

Ushirikiano huo utatumia njia ya ubunifu ya simu ya UNICEF iitwayo  U-ripoti PakAvaz, kuwawezesha vijana na wakazi wa jamii na kuimarisha maendeleo ya jamii kupitia teknolojia ya ujumbe wa simu au SMS

Nchi ya Pakistan ni mwenyeji wa wakimbizi takriban milioni 1.3 kutoka Afghanistan.

Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 64% ya idadi ya wakimbizi wa Afghanistan ni chini ya umri wa miaka 25 (pamoja na watoto chini ya umri wa miaka 18 ikiwa ni zaidi ya nusu ya idadi ya watu), na asilimia 25% ni vijana wenye umri 18-24.

Mpango huu wa kimataifa U-Ripoti PakAvaz una zaidi ya watumiaji milioni 2.8 katika nchi zaidi ya 28 kote duniani kote, ikiwa ni pamoja na Pakistan.

Mwakilishi wa UNICEF nchini Pakistan, Angela Kearney amesema kuwa kupitia ushirikiano huu, shirika lake lina matumaini makubwa katika uwezo wa U-Ripoti PakAvaz  akiongeza kuwa Pakistan  ni moja ya nchi yenye idadi ya kubwa ya vijana. Ametaja kuwa ushirikiano huu utawasaidia wakimbizi kueleweka katika maeneo ya afya, elimu, ulinzi, maji, usafi wa mazingira na ustawi wa jamii kwa njia ya matumizi ya teknolojia na simu ya mkononi.

Naye mwakilishi wa UNHCR nchini Indrika Ratwatte amebainisha kuwa kiwango hicho cha vijana wakimbizi wana uwezo wa kuleta mabadiliko kwa kutoa taarifa kuhusu masuala yanayohusiana na jamii zao kwa SMS, Twita na Facebook.