Skip to main content

Watu zaidi ya milioni 11 wanahitaji msaada Sahel-Lanzer

Watu zaidi ya milioni 11 wanahitaji msaada Sahel-Lanzer

Watu zaidi ya milioni 11 wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu , huku milioni 7.1 kati yao hawana uhakika wa chakula wakiishi kwa mlo mmoja kwa siku kwenye ukanda wa Sahel.

Hayo ni kwa mujibu wa Tobby Lanzer mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kwenye ukanda wa Sahel unaojumuisha maeneo ya Kaskazini mwa Cameroon, Magharibi mwa Chad, Kusini Mashariki mwa Niger na Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Amesema ugaidi unaendeshwa na kundi la Boko Haram ndio chachu kubwa ya hali hiyo mbaya ambayo pia imewaacha watoto zaidi ya laki tano wakiwa katika unyafuzi uliofurutu ada. Amesema kwa hiyo

(TOBBY LANZER )

“Umoja wa mataifa kwa kukabiliana na hali hiyo unashirikiana kwa karibu na uongozi wa Cameroon, Chad, Niger na Nigeria na tunatarajia kuileta pamoja jumuiya ya kimataifa kwenye mkutano utakaofanyika Oslo Februari 24, ambapo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wajumuishwa, mashirika muhimu ya kibinadamu , kama chama cha msalaba mwekundi, mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika ya Umoja wa Mataifa watashiriki ili kutoa mwanga wa zahma hii inayotokea mbele ya macho yetu , kaskazini Mashariki mwa Nigeria na ukanda mzima wa ziwa Chad”

Na kuhusu Mali Bwana Lanzer amesema ingawa hali ya usalama kiasi imeimarika lakini upande wa chakula bado ni tete

(TOBY LANZER )

“Tunatarajia watu lakini tano kutokuwa na uhakika wa chakula nchini Mali mwaka huu na hiyo ni asilimia 20 zaidi ya ilivyokuwa mwaka 2016.”