Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wathirika wa mzozo wa Sudan Kusini wapata matumaini ya elimu

Wathirika wa mzozo wa Sudan Kusini wapata matumaini ya elimu

Vijana waliolazimika kukimbia makwao kufuatia mzozo wa Sudan Kusini wamepata matumaini ya elimu kutokana na Mradi wa Udhamini wa serikali ya Ujerumani ambao unaosimamiwa na Shirika la Umoja w a Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi la (UNHCR). Taarifa kamili na John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

Mradi huo wa DAFI, ambao unadhaminiwa na serikali ya Ujerumani kwa miaka ishirini na mitano sasa, umesaidia vijana wakimbizi zaidi ya 2,000 katika nchi 41, kupata fursa ya elimu na hata kufikia tasisi za elimu ya juu. Hatua hiyo ni ya matumaini hasa ukizingatia Sudan Kusini hivi sasa inaghubikwa na vita vilivyosambaratisha maisha ya maelfu ya watu na kuwaacha watoto wengi bila elimu.

Richard Rauti ni Afisa anayehusika na mawasiliano katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Sudan Kusini.

(Sauti ya Richard)

"Bila elimu baadhi ya mambo ambayo wakimbizi wanakimbia hawatayaelewa na wakati wakipata ufahamu kupitia elimu, wanakuwa na mchango mkubwa kwa nchi zao. Kwa mfano Sudan Kusini inahifadhi watu wengi ambao walikuwa wakimbizi ambao waliishi Kakuma, DRC na Jamhuri ya Afrika ya kati, kupitia miradi kama huu wa UNHCR  watu wameweza kupata elimu na wakati wakirejea Sudan Kusini wanaweza kufanya kazi katika ofisi mbalimbali, hata mimi ninayezungumza nawe nilikuwa mwanafunzi mkimbizi."