Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi mbadala ya taka Tanzania yamulikwa

Matumizi mbadala ya taka Tanzania yamulikwa

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP Erik Solheim ametembelea Tanzania kujadili namna nchi hiyo inavyoweza kushirikiana na Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa katika ulinzi wa mazingira.

Katika ziara hiyo amekutana na Makamu wa Rais Bi. Samia Suluhu pamoja na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya makamu wa Rais anaehusika na masuala ya muungano na mazingira January Makamba na kuzuru dampo kubwa la taka la Pugu jijini Dar-es-salaam.

Waziri Makamba amesema Tanzania imepata maendeleo ya kasi katika miaka 20 iliyopita, na uwezo wa watu kununua bidhaa umeongezeka na hivyo taka zimeongezeka na hiyo ni changamoto kubwa sana, na akapendekeza ubunifu wa kushughulikia taka ikiwemo..

(Sauti ya Makamba)