Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo ya pande kinzani Syria yaanza Astana Kazakhstan

Mazungumzo ya pande kinzani Syria yaanza Astana Kazakhstan

Pande Kinzani kwenye mgogoro wa Syria zimekutana Jumatatu mjini Astana Kazakhstan, pamoja na Urusi, Uturuki na Iran ambao ni wadhamini wa mkutano huo katika mazungumzo ya kujaribu kupiga hatua ya kufikia malengo ambayo yameshindwa kutimizwa ya kumaliza miaka sita ya vita nchini Syria.

Hio ni mara ya kwanza wawakilishi wa upinzani na wa Rais Bashar al-Assad kukutana tangu mazungumzo yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa mjini Geneva kuahirishwa mapema mwaka jana.

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria Staffan de Mistura amesema Umoja huo unatuamai mazungumzo hayo yatakuwa chachu ya mazungumzo ya ana kwa ana . Mada zinazotamalaki kwenye mazungumzo hayo ni pamoja na kuimarisha usitishaji uhasama na kupiga hatua katika mazunguzo hayo itakayotoa mwanya wa mjadala zaidi hapo Februari 8 mwaka huu mjini Geneva.