Jumuiya ya kimataifa yakaribisha hitimisho la uchaguzi wa bunge Somalia

Jumuiya ya kimataifa yakaribisha hitimisho la uchaguzi wa bunge Somalia

Jumuiya ya kimataifa ukiwe mo Umoja wa mataifa, Muungano wa Afrika na IGAD wamewapongeza wajumbe wa bunge la 10 la shirikisho nchini Somalia kwa kuhitimisha uchaguzi wa wabunge, spika na manaibu spika.

Hatua hiyo ya uongozi wa bunge iliyokamilika Jumapili ndiyo inahitimisha mchakato muhimu wa uchaguzi Somalia. Jumuiya ya kimataifa imetoa wito wa wa kuanzishwa kamati ya pamoja ya uchaguzi wa Rais wa shirikisho ambayo itawezesha kufanyika kwa kura hiyo muhimu inayoshirikisha wabunge wa bunge la shirikisho na lile dogo la wananchi haraka iwezekanavyo.

Jumuiya ya kimataifa inatarajia mabunge yote mawili kushirikiana na kupanya kazi kwa amani na utulivu ili kutimiza ndoto ya Wasomali ya kujenga taifa hilo lililosambaratika kwa vita na kufikia amani ya kudumu.