Twampongeza na tutahakikisha usalama wa Jameh
Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Uchumi wa nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) na Muungano wa Afrika (AU) kwa kauli moja, umepongeza ukarimu na uzalendo wa rais wa zamani wa Gambia Yahya Jameh baada ya kuamua kuhamisha madaraka kwa Rais Adama Barrow jana jioni.
Katika tamko lao la pamoja, Umoja wa Mataifa, ECOWAS na AU umeahidi kushirikiana na serikali ya Gambia kuhakikisha rais wa zamani
Jameh
pamoja
na
familia
yake,
wafuasi wake
na wale
waliokuwa
chini
ya
uongozi wake
watapewa
hadhi,
heshima
na
usalama
nchini Gambia
na
hakutakuwa
na
kitendo
cha
vitisho
na
unyanyasaji
na
utungaji
wa
sheria
dhidi
yake
au
mali
yake
iliyo
halali.
Tamko hilo
limesema
kuwa
rais
huyo
wa
zamani
ataondoka
nchini
humo
kwa
muda
bila
ya
chuki
yoyote
ili
kusaidia
utaratibu
mzuri
na
amani
wa
uhamisho
wa
madaraka
kwa
serikali
mpya,
na
kwamba
itahakikisha
uwezo wake
wa
kurejea
nchini Gambia
wakati
wowote
atakapoamua
bila
ya
vikwazo
vyovyote.
Vile vile imesema
itahakikisha
usalama
katika
nchi
zitakazoamua
kumkaribisha
na
kumhifadhi.
Pia ECOWAS
imeahidi
kusimamisha
shughuli
zote
za
kijeshi
nchini
humo
na
wote
wameahidi
kushirikiana
na
mamlaka
ya Gambia
katika
mchakato
wa
maridhiano
na
mshikamano
wa
kitaifa.