Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Duru mpya ya mazunguzo ya Cyprus kujikita katika hakikisho la usalama

Duru mpya ya mazunguzo ya Cyprus kujikita katika hakikisho la usalama

Juhudi mpya za kumaliza mgawanyiko nchini Cyprus kwa mazungumzo baina ya pande zote zinazohusika na mustakhbali wa kisiwa hicho zimefanikiwa na zitaendelea , umesema leo Umoja wa mataifa.

Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa Mshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa Espen Barthe Eide, ambaye katika taarifa yake amesema atatoa taarifa kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Jumatatu ya Januari 23..

Masuala muhimu yalijadiliwa Mont Pelerin, yalikofanyika majadiliano hayo ambako jopo la kiufundi la wataalamu lilikutana.Mada hizo zinajumuisha hakikisho la usalama katika kisiwa hicho Mediterranean kilichogawika mapande tangu mwaka 1974.