Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni ya kupinga chuki dhidi ya Waislamu yaleta nuru

Kampeni ya kupinga chuki dhidi ya Waislamu yaleta nuru

Juma hili, katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kulifanyika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu chuki na ubaguzi dhidi ya uislamu na waislamu.

Mkutano huo wa siku moja uliandaliwa kwa pamoja na ofisi za ubalozi za Canada na Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, ujumbe wa Muungano wa Ulaya na Umoja wa nchi za kiislamu duniani, OIC.

Wakati wa mkutano huo uliolenga kuchambua madhila yanayokumba waislamu duniani, Umoja wa Mataifa ulizindua kampeni  iitwayo Pamoja yenye lengo la kukabiliana na chuki na ubaguzi dhidi ya uislamu na  waislamu duniani. Je nini kilijiri? Na ni mapendekezo yapi yalitolewa?  Tuungane basi na Flora Nducha kwa uchambuzi zaidi.