Skip to main content

Bado kuna changamoto katika maridhiano ya kitaifa Côte d’Ivoire

Bado kuna changamoto katika maridhiano ya kitaifa Côte d’Ivoire

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kujenga uwezo na ushirikiano wa kiufundi kuhusu haki za binadamu nchini Côte d’Ivoire, Mohammed Ayat, leo ametathimini changamoto za mazingira mapya ya kisiasa na kijamii nchini humo , kwa mtazamo wa kuondoka operesheni za Umoja wa Mataifa Côte d’Ivoire (UNOCI).

Katika mwisho wa ziara yake nchini humo ilianza Januari 10 hadi 17 mwaka huu Bwana. Ayat Ayat ametoa wito kwa uongozi wa nchi hiyo kufanya marekebisho bila kuchelewa katika sekta ya ulinzi na usalama, na kuimarisha taasisi kwa ajili ya amani na utawala bora kwani ni kitovu cha kufikia malengo ya dharura yaliyopangwa.

Na katika maduala ya maridhiano ya kitaifa Bwana Ayat amekumbusha kwamba suala la haki linasalia kuwa kipaumbele , hasa ukizingatia litaipeleka nchi hiyo katika ukweli na haki huku ikiheshimu na kuwahakikishia watu usawa katika kesi zao.