Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa maji wasalia changamoto kimataifa-da Silva

Ukosefu wa maji wasalia changamoto kimataifa-da Silva

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo FAO José Graziano da Silva, amesema kukuwa kwa ukosefu wa maji ni moja ya changamoto kubwa dhidi ya maendeleo endelevu, na changamoto hiyo inatarajiwa kuongezeka sambamba na ongezeko la watu duniani.

Akizungumza katika mkutano wa kimataifa kuhusu chakula na kilimo, unaoendelea mjini Berlin Ujerumani, da Silva amesema ukosefu wa maji unaathiri mamilioni ya wakulima katika nchi zinazoendelea ilihali migogoro itokanayo na rasilimali hiyo ikizidi kuwatesa watu katika kanda mbalimbali.

Amesema karibu watu bilioni moja katika maeneo yenye ukame watakabiliwa ukosefu wa maji katiaksiku za usoni, husuani maeneo ambayo yamegubikwa na umasikini na njaa.

Mkurugenzi huyo Mkuu wa FAO amesema, katika kukabiliana na changamoto hizo, jumuiya ya kimataifa imeanzisha lengo linalojitegemea kuhusu maji na hivyo akasisitiza matumizi bora ya maji na ulinzi wa rasilimali hiyo muhimu